Sera ya Faragha

MUHIMU: KWA KUTUMIA TOVUTI YETU NA PROGRAMU YOYOTE ILIYOTAYARISHWA NA WOLA. NA/AU KUTUPATIA HABARI ZAKO ZA KIBINAFSI, UNAKUBALI KWAMBA HABARI ZOTE ZA KIBINAFSI ULIZOTUMA ZINAWEZA KUTUMIWA KUTIMIZA MAKUSUDI YALIYOELEZWA KWENYE SERA YA FARAGHA IFUATAYO KULINGANA NA SHERIA NA TARATIBU ZA HABARI ZA KIBINAFSI.

Kuheshimu faragha yako

Tuna wajibu wa kulinda na kuheshimu faragha yako. Sera hii inaonyesha msingi wa kutumia taarifa zozote za kibinafsi tunazochukua kutoka kwako au zile unazotupatia katika tovuti yetu na katika programu yoyote iliyotayarishwa na Wola™. Tunahifadhi baadhi ya taarifa za msingi unapotembelea tovuti yetu na tunatambua umuhimu wa kulinda usalama wa taarifa hizo na kukujulisha tutazifanyia nini. Unaweza kuamua kutupatia taarifa zile unazoona kuwa ni taarifa za kibinafsi. Neno “taarifa za kibinafsi” linalotumiwa katika sera hii linarejelea taarifa kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, anwani ya posta, namba ya simu, au taarifa nyingine yoyote ambayo inaweza kutumiwa kukutambulisha. Neno “tovuti” linatia ndani tovuti hii na nyingine zinazohusiana na hii, kama vile wola.africa, hub.wola.africa na my.wola.africa.

Wanaotumia taarifa zako

Tovuti hii pamoja na programu yoyote iliyotayarishwa na Wola ni mali ya Wola, ambayo ni kampuni ya biafsi inayojihusisha na masuala mazima ya usambazaji wa bidhaa za lishe, urembo, uzito pamoja na usafi wa bianfsi. Ikiwa umeamua kwa hiari yako kufungua akaunti, kutoa mchango, kuomba kutembelewa, au kufanya jambo lolote ambalo linahitaji ueleze taarifa zako za kibinafsi, unaonyesha unakubaliana na Sera hii, pamoja na kukubali taarifa zako zihifadhiwe kwenye vifaa vilivyoko Marekani na taarifa zako za kibinafsi zikusanywe, zishughulikiwe, zihamishwe na kutunzwa na Wola na washirika wengine tunaohusiana nao ili kushughulikia ombi lako.

Usalama na usiri wa taarifa

Tunahakikisha kwamba taarifa zako za kibinafsi zipo salama. Mifumo yetu ya kuhifadhi na kulinda taarifa zako za kibinafsi inaboreshwa mara kwa mara ili taarifa zako zisitumiwe bila ruhusa, zisitumiwe vibaya, zisibadilishwe bila ruhusa, zisifutwe kinyume cha sheria, au zisipotee. Mtu yeyote wa tatu atakayeshughulika na taarifa zako za kibinafsi na wote wanaoshughulikia taarifa zako za kibinafsi na wana wajibu wa kuheshimu usiri wa taarifa zako. Tunatunza taarifa zako za kibinafsi kwa muda zinapohitajika tu na kwa kusudi la kukusanywa au kwa kuzingatia ripoti yoyote ya kisheria inayohusika au matakwa ya kutunza taarifa yaliyoko kwenye hati.
Tunalinda taarifa zako za kibinafsi zinapokuja kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia, kama, teknolojia ya Transport Layer Security (TLS). Tunatumia mifumo ya kompyuta inayotumiwa na watu wachache inayolindwa kielektroni kwa kutumia mikakati maalum iliyowekwa ili kulinda usiri na usalama wa taarifa za kibinafsi zinazotufikia. Tuna viwango imara vya usalama vinavyozuia matumizi yoyote ya taarifa bila kibali.

Watoto

Ikiwa wewe ni mtoto kulingana na sheria ya nchi unayoishi na unatumia tovuti yetu, unaweza kutuma taarifa zako za kibinafsi katika tovuti hii ikiwa tu utamhusisha mzazi au mlezi wako. Ikiwa wewe ni mzazi au mlezi nawe umekubali mtoto atoe taarifa za kibinafsi katika tovuti hii, unaonyesha umekubali Sera hii kwa ajili ya matumizi ya mtoto huyo. 

Taarifa kwa mtu wa tatu

Nyakati nyingine, tovuti hii na programu yoyote iliyotayarishwa na Wola zinaweza kutumia viunganishi vinavyokuelekeza kwa mtu wa tatu. Hilo linaweza kutia ndani viunganishi kwa tovuti nyingine ya mtu wa tatu (third-party) inayotoa huduma fulani kwa niaba yetu (kwa mfano, inapohusu kujaza fomu mtandaoni). Utatambua kwamba umeingia kwenye tovuti nyingine kwa sababu mwonekano wa tovuti hiyo utakuwa tofauti na anwani ya tovuti itabadilika. Kwa kuongezea, wanaweza kukutumia barua pepe au ujumbe kwenye simu yako kutokana na ombi ulilojaza katika tovuti hii na wanaweza kukujulisha kuhusu mambo ambayo ulikuwa unafanya kulingana na taarifa ulizojaza kupitia tovuti hii. Wakati tunapomchagua mtu wa tatu wa kutoa huduma, na mara kwa mara baada ya hapo, tunachunguza sera zao za faragha na za kulinda taarifa za kibinafsi ili kuhakikisha kwamba zina viwango vinavyofanana na vile tunavyotumia katika sera zetu. Hata hivyo, tovuti hizo nyingine hutoa program na huduma ambazo muundo wake, masharti ya utumiaji, sera za faragha, na mambo mengine yanayohusiana na utumiaji ambayo hatuwezi kudhibiti. Kwa sababu hiyo, utumiaji wako wa programu na huduma hizo ndani ya tovuti yetu utategemea masharti ya huduma yaliyopo wakati huo na matumizi ya tovuti hiyo kwa ujumla. Tovuti hizo zinaposasisha taarifa zao hazitujulishi, hivyo basi pitia masharti ya utumiaji kabla ya kutumia huduma zao. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera za tovuti hizo za kutoa huduma, tafadhali soma sera inayopatikana kwenye tovuti yao.

Utumiaji wako wa Huduma ya Ramani ya Google (Google Maps) katika tovuti yetu unategemea sera ya faragha ya Google; Google Privacy Policy. Google ni mtu wa tatu ambaye programu, muundo na masharti yake; Terms of Service kwa ujumla yako nje ya uwezo wetu. Kwa hiyo, utumiaji wako wa Huduma ya Ramani ya Google (Google Maps) uko chini ya Masharti Zaidi ya Huduma ya Ramani ya Google Google Maps/Google Earth Additional Terms of Service Hawatujulishi kuhusu usasishaji wa huduma zao, hivyo basi tafadhali pitia masharti ya utumiaji kabla ya kutumia huduma hiyo. Usitumie Huduma ya Ramani ya Google ikiwa hukubaliani na masharti ya utumiaji.

Kujulishwa kuhusu mabadiliko ya sera

Tunaendelea kuboresha na kuongeza utendaji mpya na mambo mengine katika tovuti hii na programu nyingine zilizotayarishwa na Wola, na pia tunaboresha na kuongeza huduma nyingine. Kwa sababu ya mabadiliko yanayoendelea, na mabadiliko ya sheria na teknolojia, tunaweza kubadili jinsi tunavyotumia habari mara kwa mara. Tukihitaji kubadili Sera yetu, tutaonyesha mabadiliko hayo kwenye ukurasa huu ili sikuzote ujue habari tunazokusanya na jinsi tunavyozitumia.

Hatijava (Active Scripting or Javascript)

Hati hutumiwa na tovuti kuboresha utendaji wa tovuti na programu yoyote iliyotayarishwa na Wola. Kutumia ufundi wa hati hutuwezesha kurejesha haraka zaidi habari ulizoomba. Hati haitumiwi kamwe na tovuti au programu yoyote iliyotayarishwa na Wola kusakinisha programu kwenye kompyuta ya mtumiaji wala kukusanya habari kutoka kwa mtumiaji pasipo idhini.

Katika tovuti yetu, ni muhimu HatiJava iwezeshwe katika kivinjari chako ili sehemu fulani za tovuti zifanye kazi ifaavyo. Vivinjari vingi humruhusu mtumiaji kuwezesha au kulemaza hati hizo katika tovuti hususa. Soma habari za msaada kuhusu kivinjari chako ili upate kujua jinsi ya kuwezesha hati katika tovuti teule.

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.
John Doe
Designer
10,000 Online Ccourses

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit.

Expert Teachers

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit.

Unlimited Access

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit.

Start Getting New Knowledge and Experience, Together!

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.